Duration 1:46:11

JUA NAMNA YA KUVUKA VIZUIZI - PASTOR SUNBELLA KYANDO & PASTOR JOHN SEMBATWA

51 650 watched
0
450
Published 5 Jul 2021

Yoshua 6:2 [2]BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Wakati Mungu anampa Yoshua maelekezo haya walikuwa bado hawajaingia Yeriko,lakini Mungu anamwambia kuwa ameshautia mji wa Yeriko katika mikono ya Yoshua.Watu wengi huwa tunaishia kusikiliza tu Mungu anasema nini juu ya maisha yetu na hatutafuti kwake kujua anataka tufanye nini ili tuweze kuona matokeo ya alichokisema. Baada ya kumwambia Yoshua hivi anampa maelekezo juu ya kuuzunguka ukuta kwa siku Saba na kisha kushangilia siku ya Saba na ukuta utaanguka. Safari ya kuuzunguka mji huwa sio rahisi kuna wakati unachoka.Ni kama ambavyo unaomba sana lakini matokeo huoni maana hata ukuta haukuanguka siku hiyohiyo.Siku ambapo ukuta unatakiwa kuanguka(siku ya Saba) walitakiwa kuuzunguka mara saba.Ni siku ambayo walichoka zaidi na waliumia zaidi lakini katikati ya uchovu na maumivu ndimo ulimokuwa ushindi wao. Unaweza ukawa unaomba sana lakini huoni matokeo,na kadri unavyoomba ndivyo ambavyo vitu vinazidi kuwa vigumu.Usikate tamaa maana ndio upo kwenye mzunguko siku ya saba,ushindi wako unakaribia.Umezunguka siku sita zote,usikate tamaa siku ya saba. Katika ibada hii Mungu kupitia Mtumishi wake Pastor Sunbella Kyando ametufundisha sana juu ya kuanguka kwa ukuta wa Yeriko,kisha tukaingia katika maombezi ambayo yaliongozwa na Watumishi wa Mungu Pastor Sunbella Kyando pamoja na Pastor John Sembatwa na Mungu alithibitisha Neno lake kwa ukubwa sana. UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322 Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Like our Facebook: https://www.facebook.com/Therealityof ... Follow our Instagram: https://www.instagram.com/realityofch ... Subscribe our YouTube: /channel/UC67L ... Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:/channel/UCyVhAzjcFaJH7lxgiMQviGQ

Category

Show more

Comments - 75