Duration 3:50

Waziri Gwajima Kuhusu Corona Nchi Yetu Sio Kisiwa, Mijadala ya Hofu, Tuikwepe

129 watched
0
0
Published 2 May 2021

“Natambua mtakuwa mnafuatilia masuala mbalimbali ya afya nchini na duniani na mtakuwa mmesikia kuwa katika nchi mbalimbali duniani changamoto ya mlipuko wa Covid-19 bado inaendelea kujitokeza na baadhi ya nchi ambazo zinaendelea kuathirika kwa kasi kubwa ni pamoja na India na Brazili. Napenda kuwahakikishia kuwa nchi yetu ilipambana vizuri sana na ugonjwa huu ulipoingia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania Machi, 2020 na kuudhibiti kwa kutumia mbinu mbalimbali kwa kadri mazingira yetu yalivyoruhusu na kuwezesha taifa kufanikiwa kuvuka vema zaidi ukilinganisha na nchi nyingine duniani”- Waziri Gwajima Ni Dhahiri kuwa mafanikio haya yalitokana na mshikamano wetu wote kitaifa kuanzia nyie wataalamu wetu wa afya pia wananchi ambao muda wote walikuwa wasikivu katika kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wa afya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali. Aidha, Wadau wetu wote walituunga mkono vikiwemo vyombo vyetu vya habari kutoa taarifa sahihi kwa wakati na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kuwa pamoja nasi katika kuomba Rehema na Neema ya Mungu ilifunike Taifa letu. Mambo yote haya yaliwezesha taifa kuwa na utulivu na kujiamini katika kupambana na mlipuko huo na hatimaye kuudhibiti. Hata hivyo nchi yetu siyo kisiwa kwani inaingiliana na jamii za nchi nyingine katika maeneo mengi ya maisha ya kila siku hivyo basi, tunaposikia taarifa hizi kupitia vyombo vya habari duniani vema nasi tukasimama imara kutumia uzoefu tuliopata katika kuudhibiti mlipuko wa awali ili kuhakikisha tunaendelea kujilinda na wimbi hili linaloendelea huko nchi zingine lisifike nchini kwetu na likifika lidhibitiwe mapema sana kwa uzoefu tulionao. “Serikali yetu kupitia sekta ya afya kwa ushirikiano na wadau wake wote iko makini kufuatilia kinachoendelea duniani na kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama na imara katika kudhibiti milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo huu wa Covid-19. Wakati masuala mbalimbali ya ufuatiliaji yakiendelea sambamba na kuchukua hatua stahiki, napenda kuwakumbusha wataalamu wote wa afya kuimarisha zaidi wajibu wetu wa kitaalamu katika kuhamasisha, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mikakati yote ya kinga na kuchukua hatua stahiki” “Natambua kuwa kazi hii ya ulinzi wa afya zetu haiwezekani bila ushirikiano na wananchi na wadau wote kwa ujumla hivyo, nitumie fursa hii kuwakumbusha tena wataalamu na wananchi wote na wadau wote kuhusu zile tahadhari muhimu ambazo tumekuwa tukielimisha mara kwa mara dhidi ya kujikinga na kudhibiti magonjwa mbalimbali ikiwemo Covid-19 kama ifuatavyo; 1. Tuepuke hofu na kuanzisha mijadala inayoleta hofu. 2. Tumairishe tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka na sabuni na iwapo maji tiririka na sabuni hakuna tutumie vipukusi (sanitizer). 3. Tuvae barakoa safi na salama ambazo tumetengeneza wenyewe au tumenunua kwa watengenezaji wa ndani waliothibitishwa na wizara ya afya. Aidha, tuvae barakoa hizo pale tunapoona tunaingia kwenye eneo lenye kuhusisha kupokea au kutoa huduma kwa mwingine aliyeko umbali wa chini ya mita moja. 4. Tufanye mazoezi mara kwa mara kwa kadri ya kila mtu alivyo kutegemeana na hali ya afya yake na mazingira yake siku hiyo. Baadhi ya mazoezi rahisi kabisa ni kutembea kwa kasi walau utoke jasho, kukimbia mwendo unaoona unakufaa, kuruka kamba, kufanya zoezi la simama-kaa na kwa watu wenye ulemavu ni kwa ushauri wa wataalamu. 5. Tufanye mabadiliko ya tabia ya lishe au vyakula tunavyotumia kwa kuhakikisha tunakula kwa wingi matunda na mbogamboga kulingana na mazingira ya vyakula vya asili katika maeneo yetu. 6. Tutambue afya zetu na tujilinde hususan wale walio katika makundi maalumu ya watu wakiwemo wenye umri mkubwa (wazee), watu wenye uzito uliopitiliza (wanene) na watu wenye magonjwa sugu (muda mrefu). Jambo hili ni muhimu sana tena sana kwani kundi hili mara nyingi ndiyo huathirika zaidi na magonjwa ya kuambukiza kutokana na hali kinga zao kuwa haziko imara zaidi. Tutatekeleza mkakati kabambe hapa kwa ajili ya kuhakikisha sekta zote zinahusika kuwafikia makundi haya na kuwalinda. Maelekezo ya mwongozo kwa makundi haya yatatolewa ikiwemo jinsi gani watatambuliwa na kuhudumia kiafya. 7. Tusisahau kutumia tiba asili zilizosajiliwa na Baraza la Tiba Asili na kama inavyoelimishwa na wataalamu husika. baraza letu la tibaasili limeendelea kusajili bidhaa mbalimbali na wizara itatoa tena orodha yake na maelezo ya upatikanaji wake. 8. Tuendelee kuepuka misongamano isiyo ya lazima ikiwemo kwenye vyombo vya usafiri hivyo, natoa wito kwa Wizara husika kusimamia jambo hili kwa kurejea mwongozo wa afya eneo husika. 9. Tuwahi kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya mara tunapoona dalili za maradhi yoyote ili watoa huduma wapate nafasi nzuri zaidi ya kugundua na kutibu na kushauri. Aidha, kila mmoja wetu ajenge tabia ya kupima afya yake mara kwa mara walau mare 4 kwa mwaka hata kama haumwi. Usisubiri unaumwa halafu unachelewa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya.

Category

Show more

Comments - 0