Duration 12:12

MAVAZI YANAYOTAKIWA BUNGENI: NAIBU SPIKA, DR TULIA ACKSON AWAFUNDA WABUNGE WANAWAKE

36 033 watched
0
133
Published 7 Jun 2021

iku za hivi karibuni umekuwepo mjadala juu ya mavazi ya wabunge baada ya mmoja wa wabunge kutolewa nje akabadili mavazi, sasa leo kumefanyika Semina kwa wabunge wanawake kuhusu uwakilishi wao bungeni pamoja na uongozi iliyoandaliwa na umoja wa wabunge wanawake kwa ufadhili wa Kituo cha sheria na haki za binadamu ambapo hoja ya mavazi ikaibuliwa na kuzungumziwa na mtoa Mada ambaye ni Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson "Ukiwa Mazingira ya bunge, ni mazingira ya uongozi ndio maana si kila mtu anaruhusiwa kujakuja hapa bungeni, ni mazingira maalumu na wewe lazima ujiweke maalumu, Bungeni sio msibani, sasa huwezi kuja bungeni kama unaenda msibani, nilimwambia mtu mmoja mfano mzuri, tunazungumza sana kuhusu mavazi, kwa kawaida hizi kanuni unaweza kuzitafsiri mpaka ukachoka sehemu ya mavazi lakini vazi linaloitwa mahsusi kwa ajili ya bunge ni lile vazi ambalo ukiambiwa umeteuliwa kuwa waziri unaitwa sasa hivi Ikulu kwenda kuapishwa utataka kurudi nyumbani kwenda kubadili au utaenda moja kwa moja kupanda gari na kwenda kuapishwa? hayo ndio maswali ya kujiuliza kabla hujatoka kuelekea bungeni kwa sababu pale ni mahali mahsusi, maalumu. Kwa hiyo hilo ndio swali la msingi kabisa kama nikiitwa ghafla naitwa mahali halafu natakiwa kukaa mbele na Rais nitaenda hivi au nitatakiwa nikabadilishe kama utatakiwa ubadilishe , badilisha kabisa kabla hujaja bungeni"-Dr. Tulia Ackson

Category

Show more

Comments - 103